Bawasiri ni nini?

BAWASIRI kitaalamu hujulikana kama HEMORRHOIDS au PILE ambayo ni hali ya kutokwa na kinyama sehemu ya njia ya haja kubwa.

Hili ni tatizo la kimmengenyo au ambalo linaweza kurithiwa na tatizo hili hushambulia sehemu ya njia ya haja kubwa na kulegeza misuli inayozunguka njia ya haja kubwa na kusababisha kutwa na damu na kupata maumivu makali sana katika eneo hilo.

Mtindo wa maisha huchangia cha tatizo hili la bawasiri Mfano: kutokunywa maji ya kutosha ambayo husababisha kukosa choo au kupata choo kigumu kinacho sababisha kusukuma nje na kuchubua kuta za misuli inayozunguka njia ya haja kubwa.

Aina za bawasiri

1. Bawasiri ya nje
Hii ni aina ya bawasiri ambayo kinyama huota na kutokezea kwa nje ya sehemu ya nje ya haja kubwa.
2. Bawasiri ya ndani
Hii ni aina bawasiri ambayo kinyama hubaki ndani ya njia ya haja kubwa bila kutokezea nje ya njia ya haja kubwa. Pia aina hii inaweza kutokezea nje wakati wa haja kubwa na kurudi baada ya kumaliza kutoa nje haja kubwa.

Hatua za bawasili

Hatua ya kwanza
Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pake pa kawaida.
Hatua ya pili
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya kujisaidia.
Hatua ya tatu
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
Hatua ya nne
Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

Athari za bawasiri ya kawaida na iliyokithri
  1. Upungufu wa damu mwilini.
  2. Kutokwa na kinyesi bila kijitambua kama vile mgonjwa wa “Anal fistula”
  3. Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
  4. Kupungukia nguvu za kiume kwa jinsia ya kiume.
  5. Kupata maumivu sana sehemu ya njia ta haja kubwa.
Vyanzo vya bawasiri
  1. Changamoto ya kukosa choo au kupata choo kigumu.
  2. Tatizo sugu la kuharisha.
  3. Kunyanyua vitu vizito.
  4. Mazingira ya kuketi sehemu moja kwa muda mrefu bila kunyanyuka mfano; madereva wa masafa marefu.
  5. Uzito wa mwili kupita kiasi.
  6. Ngono kinyume na maumbile(Anal sex).
Ushauri wa namba ya kuepukana na bawasiri
  1. Tumia mboga za majani kwa wingi.
  2. Tumia matunda kwa wingi.
  3. Tumia maji ya kutosha angalau glasi 4-6 za maji kwa siku.
  4. Tumia nafaka zisizo kobolewa.
  5. Jiepushe na ngono za nyuma ya maumbile.
  6. Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu.
  7. Jiepushe na matumizi ya choo cha kukaa kwasababu kinaongeza shinikizo la damu kwenye mishipa ya tundu la haja kubwa na kusababisha bawasiri kuvimba na kuongezeka.
  8. Tibu changamoto ya vidonda vya tumbo kwasababu inasababisha kukosa choo na kupata choo kigumu ambacho kinaingeza ukubwa wa tatizo la bawasiri.
Dalili za bawasiri
  1. kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa.
  2. kujitokeza kwa kinyama eneo la haja kubwa.
  3. kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa.
  4. kupata kinyesi chenye damu.
  5. kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia na kutoka damu.
  6. Kupata choo chenye damu au chenye kunuka DAMU.

Tiba yetu imewashangaza wengi kwa jinsi inavyo tibu bawasiri kwa haraka ndani ya siku 3 hadi 7. Tiba hii inakufikia popote ulipo.