Ugonjwa wa kisukari ni nini?
Ugonjwa wa kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu iliyomo mwilini inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu.
Aina za kisukari
- Kisukari kinachotegemea insulini/ kisukari cha kuanzia udogoni au “type one diabetes”
- Kisukari kisichotegemea insulini/ Kisukari cha ukubwani au “type two diabetes”
Kisukari kinachotegemea isulini
Hiki ni kisukari ambacho hutokea wakati mwili unaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulini ambacho huuwezesha mwili kutumia sukari. Kisukari cha aina hii huweza kudhibitiwa kwa kutumia sindano za insulini pamoja na kurekebisha ulaji. Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji, au kwa kurekebisha ulaji pekee.
Dalili za ugonjwa wa kisukari
- Kukojoa mara kwa mara
- Kusikia kiu sana
- Kusikia njaa sana
- Kuchoka sana bila kufanya shughuli yoyote.
- Kukosa nguvu
- Kupungua uzito kwa kiwango kikubwa bila kukusudia
- Kizunguzungu
Mambo ya kufanya unapokuwa na ugonjwa wa kisukari
Kudhibiti ulaji wako kwa kufuatisha ulaji unaofaa yaani ulaji unaokuwezesha kutosheleza mahitaji ya mwili wako kiafya na kukuwezesha kuwa na uzito unaostahili, pamoja na kuhakikisha sukari mwilini inakuwa katika kiwango kinachokubalika kwa afya bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia aina na kiasi cha chakula unachokula. Pia ni vyema ukawa makini na njia zinazotumika kuandaa chakula.
Ushauri
- Epuka unywaji wa pombe kwani unaweza kukuletea athari mwilini.
- Epuka uvutaji wa sigara na bidhaa za tumbaku na madawa ya kulevya, kwani huathiri afya yako.
- Epuka msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi au
- kushiriki katika matukio salama yanayokufurahisha.
- Kula chakula cha mchanganyiko, hata hivyo zingatia kiasi na aina ya chakula kwa kuangalia hasa kiasi cha sukari na mafuta yaliyotumika katika mapishi.
- Kula milo kamili mitatu kwa siku na asusa zenye virutubishi vingi muhimu kati ya mlo mmoja na mlo unaofuata.
- Kula kiasi kidogo cha vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi kwa mfano wali, ugali, viazi, mihogo, ndizi, magimbi n.k.
Mambo muhimu ya kuzingatia
- Tumia nafaka isiyokobolewa kwa mfano dona na ngano.
- Kula mbogamboga kwa wingi kwa mfano mchicha, matembele, majani ya maboga, karoti, biringanya, kisamvu, mlenda n.k
- Kula vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi kama vile maharagwe, njegere, mbaazi, kunde, choroko n.k (tumia kama kitoweo).
- Kula matunda kwa kiasi kwa mfano ndizi au chungwa moja au kipande kidogo cha embe kubwa au papai katika kila mlo.
- Kunywa maji kwa wingi.
- Epuka kutumia vinywaji na vyakula vyenye sukari nyingi kama jamu, asali, visheti, futari ya sukari, soda, chokoleti, pipi, bazoka, barafu na juisi za kusindikwa viwandani.
- Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi au chumvi nyingi.
- Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara angalau kwa nusu saa kila siku, kwani husaidia mzunguko wa damu na kukufanya uwe na afya nzuri.
Zingatia kanuni za afya zifuatazo
- Piga mswaki kila baada ya kula au angalau mara mbili kwa siku.
- Kuwa msafi wa mwili na mavazi
- Tunza miguu yako kwa makini kuzuia kupata majeraha.
- Kausha vizuri maji katikati ya vidole vya miguuni.
- Epuka kujiumiza mwilini.
- Vaa viatu na soksi zisizobana kila wakati.
- Inashauriwa kuvaa viatu vya wazi
- Kutimiza masharti ya dawa na ulaji
- Kuhudhuria kliniki za kisukari kwa kufuata ratiba uliyopangiwa.
- Kumuona daktari mapema mara unapopata tatizo lolote la kiafya.
- Kupata taarifa sahihi na elimu kuhusu kisukari kutoka kwa wataalamu wa afya.
Mambo ya kuzingatia:-
- Punguza uzito mkubwa ikiwa una uzito mkubwa.
- Usiache matibabu bila ushauri wa daktari.
- Usikae bila kula kwa mda mrefu.
Kuna hali za aina mbili ambazo kila mgonjwa wa kisukari, familia au waalimu wanapaswa kujua na kuchukua tahadhari kubwa zinapojitokeza:-
- Kiwango cha sukari katika damu kinaposhuka.
- Kiwango cha sukari katika damu kinapopanda.
Hatua za haraka inabidi zichukuliwe kumsaidia mgonjwa, kwani anaweza kupoteza fahamu na hata maisha.
Hali hii hutokea wakati kiwango cha sukari kinapokuwa chini kuliko kawaida. Hii inaweza kutokana na kutumia dawa kuzidi kipimo, kunywa pombe, kufanya mazoezi bila kula, kufanya mazoezi yanayotumia nguvu kwa muda mrefu, au kukaa bila kula kwa muda mrefu.
– Moyo kwenda mbio
– Mwili kutetemeka
– Kusikia njaa
– Kizunguzungu
– Kuona mbilimbili (double vision)
– Kuchanganyikiwa
– Kutokwa jasho kwa wingi
– Kuchoka sana
Hali hii ikizidi mgonjwa huweza kupoteza fahamu. Mgonjwa akipatwa na hali hii apewe kitu chenye sukari kama vile sukari, glukosi, soda au juisi.
Hali hii hutokea wakati kiwango cha sukari kinapokuwa juu kuliko kawaida. Hii inaweza kutokea wakati mgonjwa anapoacha kutumia dawa, anapoacha kufuata masharti ya ulaji unaotakiwa, anapopata maambukizo au maradhi mfano, malaria, mafua, Pneumonia n.k
– Kupumua haraka haraka
– Kuongezeka mapigo ya moyo
Hali hii ikizidi mgonjwa hupoteza fahamu na hatimaye maisha kama hatapata matibabu mapema.
Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe chochote isipokuwa afikishwe kituo cha afya.
- Kupungua kwa uwezo wa kuona na hata upofu.
- Figo kutofanya kazi vizuri.
- Vidonda vya miguuni kutopona na hata kusababisha kukatwa
- kidole au mguu
- Maradhi ya moyo.
- Kufa ganzi na kupoteza hisia hasa mikononi na miguuni
- Kiharusi
- Kupungua kwa nguvu za kiume.
- Waalimu washirikiane na wazazi au walezi kuhakikisha mtoto anapata asusa zenye virutubishi muhimu anapokuwa shuleni.
- Asaidiwe kuepuka vyakula visivyo na ubora kama vile vyenye
- sukari nyingi, chumvi nyingi au mafuta mengi.
- Afikiriwe wakati wa michezo, mazoezi na kazi za kutumia
- nguvu ili kiwango cha sukari mwilini kisishuke kupita kiasi.
- Aangaliwe ili aweze kuzingatia masharti ya kula na kutumia dawa
- Wewe ni nguzo muhimu katika kumudu kisukari na uamuzi wako juu ya matibuba ndio usalama wako. Ikubali hali yako na tafuta ushauri wa kitaalam. Jikinge na madhara yaletwayo na kisukari. Fuata ushauri unaopewa na wataalam wakati wote. Mtoto anayetumia insulini inabidi awe makini na ulaji wake, hususan akiwa shuleni na, Aelimishwe kuhusu dalili za mwanzo za kushuka au kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu, azingatie na aoanishe muda wa kupata sindano ya insulini na muda wa kula.