Lishe kwa mama na mtoto
Lishe bora kwa mama na mtoto ni hali ya afya anayokuwa nayo mama na mtoto kama matokeo ya kula chakula kinachotokana mlo kamili yaani makundi matano ya vyakula ambayo ni (nafaka, mizizi na ndizi mbichi), asilia ya wanyama na jamii ya mikunde, Mboga za majani, Matunda, (Sukari, mafuta na asali mbichi).
Ni muhimu sana kuzingatia swala la kiasi cha chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kusaidia mwili kukua vizuri na mama au mtoto kuweza kujikinga na mgonjwa.
Lishe kwa mama mjamzito
Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu sana kwa sababu humpatia mama virutubishi muhimu kulingana na hali yake. Wakati wa ujauzito mama anahitaji virutubishi zaidi kwa ajili ya maendeleo yake kiafya pamoja na mtoto aliyetumboni.
Ni muhimu kutamvua kuwa mahitaji ya virutubishi kwa mama mjamzito huongezeka kwasababu na mtoto huitaji zaidi virutubishi katika kukamilisha uumbwaji wake tumboni na ndio maana wazazi wengi wasiyo zingatia lishe bora
kwa mama mjamzito huwa hatarini kujifungua watoto wenye changamoto za afya zinazo sababiswa na kutokamilika kwa uumbwaji wa baadhi ya viungo vya mwili au ubongo(akili).
Lishe bora huimarisha afya ya mama na humsaidia mtoto kukuwa vizuri kimwili na kiakili.
- Mama kutoongezeka uzito kama inavyotakiwa na hivyo kukosa nguvu, kupata maumivi ya mgongo, n.k
- Upungufu wa damu wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ambao huweza kusababisha hata kifo.
- Uwezekano wa mimba kuharibika.
- Mtoto kufia tumboni.
- Kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu.
- Kuzaa mtoto njiti au kuzaa mtoto.
- Kuongezeka kwa magonjwa kwa sababu ya mfumo wa kinga kuwa dhaifu
- Kujifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa.
- Kujifungua mtoto mwenye mgongo wazi
10. Kujifungua mtoto mwenye mdomo wa sungura.
Matatizo haya yanaweza kumpata yeyote.
Matatizo haya yanazuilika kwa kuzingatia kanuni za lishe bora kwa mama mjamzito katika kipindi chote cha ujauzito.
- Kula milo minne kwa siku na asusa au vitafunwa mara nyingi kadri uwezavyo hii itakuwezesha kuupa mwili nguvu na lishe ya kutosha kwa ajili yako na mtoto anayekua tumboni.
- Hakikisha mlo wako unakuwa na vyakula mchanganyiko vinavyopatikana katika makundi matano ya vyakula.
- Asusa au vitafunwa vinaweza kuwa vitu kama vile mahindi ya kuchoma au kuchemsha, kikombe cha maziwa, viazi, mayai, karanga, matunda n.k.
- Epuka kunywa kahawa au chai wakati wa mlo kwani huingiliana na ufyonzwaji wa virutubisho katika mwili.
- Meza vidonge vya kuongeza damu (FEFO) kulingana na ushauri uliyopewa katika mahudhurio ya kliniki ya wajawazito.
- Kuongeza ulaji wa vyakula vyenye asili ya wanyama mfano nyama, kuku, samaki, dagaa n.k. Vyakula vya asili ya wanyama na mboga za majani na matunda huongeza damu kwa haraka zaidi.
- Kula matunda ya aina mbali mbali lakini epuka matumizi ya papai na nanasi kama haujapata ushauri mzuri kutika kwa mtaalam.
- Kula mboga za majani kwa wingi kila siku.
- Tumia vyakula vilivyoongezwa virutubishi(fortifiend products) kwa mfano chumvi iliyoongezewa madini joto, mafuta ya kula yaliyoongezew Vitamin A, unga wa mahindi n.k
- Kunywa maji ya kutosha kila siku (angalau glasi 6- 8 au lita 1.5-3).
- Jikinge na Malaria kwa kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa.
- Tumia dawa za kuzuia minyoo kama inavyoshauriwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
- Jikinge na maambukizi ya magonjwa ya ngono na virusi vya UKIMWI na kama tayari ni mwasirika fika kliniki ya wajawazito upewe mwongozo wa namna ya kumkinga na kumlinda mtoto aliye tumboni ili asipate maambukizi ya UKIMWI.
- Epuka utumiaji wa sigara na pombe kwasababu inaathiri na kuia matumizi ya virutubishi na afya ya mama na mtoto.
- Kuanza kliniki mapema mara tu ya kujihisi mjamzito na uendelee kuhudhuria ili kupata huduma na ushauri bora zaidi.
Mama unayenyonyesha unatakiwa kupata Lishe bora kulingana hali ya mwili kwa kipindi cha unyonyeshaji ili kuongeza kiwango cha uzalishaji maziwa ya kutosha kwa ajili ya unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama peke yake kwa kipindi cha miezi 6 sita peke yake tu.
Kwa sababu hiyo, ni muhimu mama anayenyonyesha kula mlo kamili zaidi ya mitatu kwa siku na asusa kati ya mlo na mlo.
- Itakausaidia kuwa na afya bora kwasababu itakupatia virutubishi vya kutosha kutokana na ongezeko la mahitaji ya virutubishi wakati wa unyonyeshaji.
- Itausaidia mwili kutengeneza na kutoa maziwa ya kutosha kadri mtoto anavyohitaji.
- Itakusaidia kuimarisha kinga zako za mwili na kinga za mtoto ambazo mtoto anazipata kupitia maziwa yako wakati kunyonyeshwa.
- Itakusaidia kuzuia upungufu wa damu kwa mama na mtoto.
- Itakusaidia kumwezesha mtoto kuwa na afya bora kutokana na kupata maziwa ya kutosha kutoka kwa mama.
- Kula milo kamili zaidi ya mitatu kwa siku, mlo kamili ni mlo wenye chakula mchanganyiko angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la chakula(makundi matano).
- Kula chakula kingi na cha kutoshakatika kila mlo.
- Kula asusa kati ya mlo na mlo.
- Kumeza vidonge vya kuongeza damu (FEFO) kwa kipindi cha miezi 3 baada ya kujifungua.
- Kutumia vyakula vilivyoongezwa virutibishi, kama vile mafuta ya kupikia yaliyoongezewa Vitamin A, Chumvi iliyoongezewa madini Joto, unga wa ngano, unga wa mahindi n.k
- Kuongeza ulaji wa vyakula vyenye asili ya wanyama mfano nyama, kuku, mayai, maziwa, samaki, dagaa n.k. Vyakula vya asili ya wanyama vina virutubishi vya aina mbalimbali kwa wingi ikiwemo madini chuma ambayo husaidia kuongeza damu mwilini.
- Kula matunda yenye rangi mbalimbali mbali mbali.
- Kula mbogamboga kwa wingi.
- Kunywa maji ya kutosha kila siku (angalau glasi 8 au lita 1.5-3).
- Kujikinga na Malaria kwa kulala kwenye vyandarua vilivyowekwa dawa kila siku.
- Kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi vya UKIMWI
Pia ni muhimu mama anayenyonyesha kusaidiwa kazi nzito ili apate muda wa kutosha wa kupumzika na kumnyonyesha mtoto mara kwa mara kila anapohitaji, usiku na mchana.
Kumbuka; Mtoto anyonyeshwe kila mara anapohitaji kunyonya au angalau kila baada ya masaa matatu.
Hii hali ambayo imekuwa ikiwakumba wakina mama wengi lakini ni pia ni changamoto inayotatulika kwa hara na kwa urahisi sana endapo mama atazijua mbinu za kuepuka changamoto hii kulingana na chanzo cha tatizo lake.
Hali hii imekuwa ikuwakumba watoto wengi na kuwafanya wazazi wengi na walezi kuwa na msongo wa mawazo juu ya namna ya kuwasaidia watoto kuongezeka uzito.
Kwasababu mtoto mwenye uzito pungufu ni kiashiria cha udumavu na husababisha mtoto kushuka kinga za mwili na kuugua mara na kudumaa kiakili.
Hali hii husababishwa na vyanzo vingi sana kama vile aina ya mapishi vyakula anavyoandaliwa mtoto, Mzio(Allergy), Ugonjwa mfano: Vidonda vya mdomoni, n.k
Aina ya ulishaji, Maandalizi ya vyakula, Kiasi cha vyakula, n.k
Tatizo hili linawatesa sana wototo wengi wachanga kwa wadogo na ni tatizo linalo tatulika kwa urahisi sana endapo mama au mlezi atafuata hatua elekezi kutoka kwa mtaalam wa afya kulingana na chanzo cha tatizo la kukosa choo.