Shinikizo la damu (presha)
Kwa kawaida kila mwanadamu anashinikizo la damu kwasababu shinikizo la damu ndio husaidia damu kusukumwa na moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili.
Hivyo shinikizo la damu ni nguvu inayotumika kusukuma damu kwenda viungo mbalimbali vya mwili na tishu mbalimbali za mwili.
Aina ya shinikizo la damu:
a) Shinikizo la juu la damu.
b)Shinikizo la chini la damu.
Shinikizo la juu la damu/presha ya kupanda (hypertension)
Hutokea panapokuwa na ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini. Ukubwa washinikizo hilo la damu unategemea wingi na nguvu ya msukumo wa damu kutoka kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu mwilini. Kifaa maalum hutumika kupima shinikizo la damu na kiwango kinachochukuliwa kuwa cha kawaida ni 120/80 mmHg au chini yake.
Lakini chini ya 120/80mmHg huashiria shikizo la chini la damu ambalo ni kinyume cha shinikizo kubwa la damu. Pale kiwango kinapokuawa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo hutambulika kama shinikizo kubwa la damu, kama inavyoelezwa katika mwongozo wa viwango vya shinikizo la damu.
Hata hivyo panaweza kuwepo tofauti kati ya mtu na mtu. 121/80mmHg na 139/89mmHg hivi ni vipimo vya mwanzo ambavyo huweza kuonesha kuwa mgonjwa ana shinikizo la juu la damu au Presha ya kupanda. 140/90mmHg na zaidi ni vipomo vinavyo ashiria shinikizo la juu la damu.
- Kizunguzungu.
- Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara hususani sehemu ya kisogo.
- Baadhi kutokwa na damu puani.
- Baadhi kupata maumivu ya kifua.
- Mapigo ya moyo kwenda mbio wakati umepumzika.
- Kupata uchovu wa mara kwa mara.
- Fuata mtindo bora wa maisha.
- Epuka vyakula vyenye mafuta mengi na chumvi nyingi.
- Epuka mafuta yanayotokana na asili ya wanyama.
- Epuka vyakula vyenye lehemu kwa kiasi kikubwa.
- Punguza kiasi cha nyama unachokula hasa nyama nyekundu;
- Punguza uzito uliyozidi au epuka uzito uliozidi.
- Epuka matumizi ya pombe, sigara na tumbaku.
- Ondoa Ana na msongo wa mawazo.
- Fanya mazoezi angalau dakika 30-45 kwa siku au angalau mara tatu kwa wiki.
- Uzito mkubwa kupita kiasi.
- Msongo wa mawazo.
- Kuwepo na matatizo mengine ya kiafya mwilini, kama magonjwa ya figo, matatizo ya mishipa ya damu, magonjwa ya moyo, matatizo ya vichocheo mwilini, kisukari au saratani.
- Matumizi ya chumvi kwa wingi au vyakula vyenye chumvi nyingi
- Matumizi ya baadhi ya madawa.
- Kuwa na msongo wa mawazo.
- Kuwa na historia ya shinikizo kubwa la damu katika familia ya mgonjwa.
- Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40.
- Jinsia ya kiume iko hatarini sana kuliko jinsia ya kike.
- Kutofuata mtindo bora wa maisha mfano uvutaji wa sigara n.k
- Tatizo hili huweza pia kujitokeza kipindi cha ujauzito.
- Magonjwa ya figo.
- Magonjwa ya moyo (moyo kuwa mkubwa, moyo kushindwa kufanya kazi).
- Uharibifu wa macho (retina) na kushindwa kuona.
- Kisukari.
- Kiharusi.
- Kifo