Vidonda vya tumbo ni nini?
Ni hali ya kuwa na vidonda sehemu mbalimbali ya mfumo wa mmengenyo wa chakula hususani maeneo ya ndani ya tumbo, Umio, na sehemu ya chini ya tumbo(duodenum).
Vidonda vya tumbo vinaweza kusababishwa na kushambuliwa na bakteria aina ya Helicobacter Pylori(H.Pylori), Kuunguzwa na tindikali au asidi kwenye mfumo wa mmengenyo wa chakula kutoka na vyanzo mbalimbali ambavyo hupelekea kupata vidonda vya mfumo wa mmengenyo mfano kooni au sehemu ya umio, tumboni, na sehemu ya chini ya tumbo.
Aina za vidonda vya tumbo:
Peptic Ulcers ni aina ya vidonda vya tumbo ambavyo huathri ndani ya kitambaa cha tumbo au utumbo mdogo na mara nyingi ni matokeo ya maambukizo ya bacteria anayeitwa Helicobacter Pylori yaani kwa kifupi H. Pylori pia huweza kusababishwa na utumiaji mkubwa wa dawa ya kuzuia maumivu.
Vidonda vya peptic vinaweza kusababisha kiungulia, maumivu ndani ya tumbo, kichefuchefu, kupoteza uzito, na dalili zingine.
Duodenal Ulcers ni aina ya vidonda vya tumbo ambavyo huathri kwenye utumbo mdogo wa juu. Dalili ya kawaida ya vidonda hivi ni maumivu makali juu wa tumbo hususani wakati tumbo likiwa ni tupu au ukiwa na njaa.
Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyo tokea maeneo ya kifuani kwenye umio na husababisha dalili za maumivu makali ya kifua mithiri ya chembe ya moyo, Maumivu makali ya mabega kuelekea kwenye mgongo na kujisikia kuchoka mara kwa mara.
Vyanzo vya vidonda vya tumbo
1. Msongo wa mawazo(stresses).Watu wengi wamepata vidonda vya tumbo kutokana na hiki chanzo kwa sababu ubongo/ilipo pituitary gland unapokosa uwezo mzuri wa kuratibu vichocheo/hormones na vimeng’enya/enzymes za chakula husababisha kuzalishwa kwa wingi asidi/tindikali(Acid) ndani ya tumbo na hivyo kulipelekea tumbo kuunguzwa na kupata madonda ya tumbo. Bakteria aina ya Helicobacter Pylori(H.pylori).
2. Mazingira.
3. kukosa ratiba maalum ya kula chakula.
4. Matumizi ya madawa ya maumivu bila mpangilio.
Dalili za vidonda vya tumbo ni zifuatazo:-
- Kupata maumivi ya mgongo na mabega au kiuno.
- Mapigo ya moyo kuongezeka kama vile moyo unataka kutoka.
- Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kiume kwa wanaume.
- Kukosa usingizi au kupata usingizi wa mara kwa mara.
- Maumivu makali sehemu za kifuani kwa ndani kama vile unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.
- Tumbo kujaa gesi.
- Tumbo kuwaka moto.
- Maumivu makali sehemu vilipo vidonda vya tumbo.
- Kukosa choo au kupata choo kigumu.
- Kukosa hamu ya kula
- Kabisa au kula na kushiba haraka.
- Kupata choo Chenye damu.
Madhara yanayotokana na vidonda vya tumbo ni yafuatayo:-
- Kuvuja damu ndani ya mwili .
- Upungufu wa damu (Anemia).
- Kupata kinyesi cheusi kama cha mbuzi au chekundu.
- Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
- Shida katika kupumua
Saratani ya tumbo (Stomach cancer). - Kutapika damu.
- Msongo wa mawazo (stress).
- Kupungua kwa nguvu za kiume.